10 Machi 2022 - 20:20
Waturuki wachoma moto bendera za Wazayuni kulaani safari ya Rais wa Israel

Wananchi wa Uturuki wamefanya maandamano makubwa ya kupinga na kulaani safari ya Isaac Herzog, rais wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel nchini humo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Katika maandamano hayo ya jana Jumatano, wananchi wa Uturuki waliokuwa wamekusanyika katika Medani ya Taksim walichoma moto bendera za utawala haramu wa Israel, na kulaani safari hiyo ya siku mbili ya rais wa utawala dhalimu wa Israel.

Baadhi ya waandamanaji walikuwa wamebeba mabango yenye jumbe za kuulaani utawala katili wa Israel, huku wengine wakisikika wakipiga nara za "Mauti kwa Israel" na "Mauti kwa Marekani."

Waandamanaji hao wamesema safari ya Rais wa Israel nchini Uturuki ni pigo kwa umma wote wa Kiislamu na hususan wananchi madhulumu wa Palestina wanaopigania uhuru wao.

Wananchi wa Uturuki wamekosoa vikali njama zozote za kutaka kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel, na wamesisitiza kuwa wataendelea kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina.

342/