Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Akizungumza mbele ya wafuasi wake katika mji wa Ohio, Trump amsema, Joe Biden kutoka chama cha Democratic anapokea amri kutoka kwa "Sungura wa Pasaka" na hachukui maamuzi kwa hiari yake.
Amesema, hadi hivi sasa katika historia ya Marekani hakujawahi kuwa na rais dhaifu kama huyu ambaye hajui chochote kinachoendelea si ndani wala nje ya Marekani.
Rais huyo wa zamani wa Marekani ameongeza kuwa, hivi sasa nchi hiyo inaelekea kusambaratika kabisa na Biden hajui hata anakoipeleka nchi. Unamuona anakwenda huku na huko bila ya malengo maalumu.
Ikumbukwe kuwa hata hivi karibuni wakati Joe Biden alipokuwa anahutubia alipomaliza alinyoosha mkono kusalimiana na hewa kwa sababu hakukuwa na mtu yeyote pembeni yake na hicho kinahesabiwa ni katika vituko vikubwa vya rais huyo kizee wa Marekani.
Biden amekuwa akitoa matamshi ya ajabu ajabu mara kwa mara kiasi kwamba, hivi karibuni, mashirika ya kijasusi ya Marekani yalimkana rais huyo na kusema, madai yake kuwa Russia imefanya mauaji ya kimbari nchini Ukraine, ameyatoa mwenyewe tu na hayana ushahidi wowote.
Televisheni ya NBC litangaza habari hiyo na kusema kuwa, maafisa wa serikali ya Biden ndio waliotangaza kwamba, ripoti za mashirika ya kijasusi ya Marekani yameshindwa kupata ushahdi wa madai ya rais wa nchi hiyo, Joe Biden kuwa Russia imefanya mauaji ya kimbari nchini Ukraine.
342/