4 Desemba 2022 - 19:01
Virusi vya Influenza vyaenea katika majimbo 44 ya Marekani

Takwimu mpya kutoka Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini Marekani (CDC) zinaonyesha kuwa mwaka huu, nchi hiyo imekabiliwa na wimbi kubwa la virusi vya homa ya mafua (Influenza).

Kwa kawaida msimu wa mafua ya Influenza huanza katika mwezi Disemba huko Marekani; na maambukizi huongezeka zaidi katika miezi ya Januari au Februari,  lakini mwaka huu ugonjwa huo umeenea haraka hna kwasi kubwa. 

Kituo cha  Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini Marekani kimetangaza kuwa wiki iliyopita majimbo 44 yaliripoti maambukizi ya homa ya mafua ya Influenza. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wagonjwa wasiopungua 19,593 walilazwa hospitalini wiki iliyopita baada ya kudhihirisha dalili za ugonjwa huo. 

Takwimu za CDC pia zinasema, hadi sasa watoto wawili wameaga dunia baada ya kuambukizwa Influenza na kiujumla watu 14 wamepoteza maisha katika msimu huu kwa ugonjwa huo nchini humo. 

Sambamba na kuenea kwa virusi vya homa ya mafua na muendelezo wa maambukizi ya Covid-19 miongoni mwa watoto nchini Marekani, mamlaka ya afya imeandikia barua ikimtaka Rais Joe Biden na Waziri wa Afya kutopinga tamko la hali ya dharura, lakini Ikulu ya White House imepinga ombi la mashirika ya afya ya watoto ya kutangazwa hali ya hatari ya dharura ya kitaifa.

342/