Akikiri kushindwa shirika hilo katika majukumu yake ya kusimamia na kusambaza chakula kwa wahitaji duniani, David Beasley amesema: "Licha ya kuwa tumeweza kufikisha misaada ya chakula na kulisha mamilioni ya watu ulimwenguni, lakini ukweli wa mambo ni kwamba hatujaweza kuwalisha wote walio na njaa na hivyo maafa ya njaa kali bado yanaendelea kushuhudiwa katika ulimwengu uliojaa utajiri.
Beasley pia ametangaza katika taarifa kwamba ataacha kazi mnamo Aprili mwaka ujao wa 2023 mwishoni mwa kipindi chake cha miaka sita.
Mkurugenzi Mtendaji huyo wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani amesema: "Kuhudumu katika sekta hii kumeniletea furaha kubwa na ni jambo linalotia uchungu mkubwa maishani mwangu kwamba ninaondoka kwenye nafasi hii."
David Beasley aliteuliwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Mpango wa Chakula Duniani wa Umoja wa Mataifa na Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani, mnamo 2017.
Mashirika ya kimataifa yametahadharisha hivi karibuni kuhusu ongezeko la idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani mwanzoni mwa mwaka ujao 2023 na kulitaja kuwa moja ya matokeo ya vita vya Ukraine na athari mbaya za mabadiliko ya hali ya hewa kwa baadhi ya nchi za Afrika na Asia.
342/