Miezi kumi inapita sasa tangu Russia ianzishe oparesheni maalumu ya kijeshi huko Ukraine mwanzoni mwa mwaka huu. Russia ilitangaza mapema kwamba, itasitisha vita huko Ukraine kama itapewa dhamana na kuhakikishwa kwamba Ukraine si tishio la kijeshi, na vilevile kuondoka madarakani Wanazi Mamboleo katika nchi hiyo ya Ulaya Mashariki.
Sergei Lavrov amesema kuwa, Rais Volodymyr Zelenskyy wa Ukraine amesema katika ziara yake ya karibuni nchini Marekani kuwa kwamba: "Amani ya kiadilifu haina maana ya maelewano. Lavrov amesema: Hiki kwa hakika ndicho wanachokitaka ili kutoa pigo kwa Russia katika medani za vita na katika masuala ya kistratejia.
Lavrov lengo la nchi za Magharibi ni kuziweka kizuizini nchi nyingine, hata hivyo akthari ya nchi zinatambua na kuelewa vyema suala hili.
Matamshi hayo ya Lavrov yametolewa katika hali ambayo Meja Jenerali Kyrylo Budanov Mkuu wa Idara Kuu ya Ujasusi ya Wizara ya Ulinzi ya Ukraine amesema kuwa, nchi hiyo itaikomboa Crimea kwa kutumia diplomasia na nguvu za kijeshi. Meja Jenerali Budanov ameongeza kuwa, hakuna kitu kinachoweza kufanyika bila ya kutumia nguvu na kwamba vikosi vya jeshi la Ukraine vitaelekea huko Crimea vikiwa na silaha mkononi.
Afisa huyo wa ngazi ya juu wa intelijinsia wa Ukraine amedai kuwa, Kiev haitaraji kufanya mabadiliko ya msingi katika medani ya vita katika msimu wa baridi licha ya Russia kuwa katika hali ya mkwamo hivi sasa.
342/