Katika mazungumzo yaliyofanyika hivi karibuni kati ya Iran na Saudi Arabia mjini Beijing, China nchi hizo mbili zilikubaliana kurejesha uhusiano wa kidiplomasia baada ya miaka saba. Kwa mujibu wa gazeti la Rai Alyoum, Ahmed Abul Ghait, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema katika mkutano na waandishi wa habari hapo jana baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Lebanon, Najib Mikati mjini Beirut ya kwamba: “kikao cha viongozi wa nchi za Kiarabu kitafanyika mwezi Mei ujao nchini Saudi Arabia. Kuhusu mapatano yaliyofikiwa katika ya Iran na Saudi Arabia, Abol Ghait amesema, "makubaliano haya ni 'chanya kwa maana halisi'."Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amefafanua kuwa "athari za awali za makubaliano yaliyofikiwa kati ya Saudia na Iran ni kupatikana aina fulani ya uthabiti wa kisiasa na kiusalama kati ya nchi hizo mbili, lakini athari zake katika masuala mengine ya eneo bado hazijabainika."Tarehe 3 Januari 2016, Saudi Arabia ilivunja uhusiano wake wa kidiplomasia na Iran kwa kisingizio cha baadhi ya watu kushambulia ubalozi wake mkuu mjini Tehran na ubalozi wake mdogo katika mji wa Mashhad.../
342/