Kwanza ni mshikamano ambao uliibuka kati ya pande tofauti za mhimili wa muqawama au mapambano. Huu ni mshikamano ambao ulidhihirika baada ya mashambulio ya hivi karibuni ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al –Aqsa. Makundi ya muqawama huko Palestina na Lebanon yalijibu jinai hiyo kwa mashambulizi ya pamoja dhidi ya Israel.
Yoav Gallant Waziri wa Vita vya Utawala wa Kizayuni wa Israel amekiri kwamba utawala huo sasa unakabiliwa na changamoto mpya kutoka kwa harakati za muqawama.
Matamshi hayo yametolewa baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kutangaza kuanguka kwa moja ya ndege zake zisizo na rubani wakati wa uvamizi wa anga ya Syria.
Kwa mujibu wa gazeti la Israel "Yadiyot Aharanot", msemaji wa jeshi la Israel alidai Jumatano iliyopita kwamba ndege ya jeshi la utawala huo ilianguka katika eneo la Syria wakati ilipokuwa ikiruka katika anga ya nchi hiyo Jumanne usiku. Ben Kinon alisema kuwa chanzo cha suala hilo kinachunguzwa na amejiepusha kutaja aina ya ndege isiyo na rubani iliyoanguka nchini Syria na kudai kuwa hakuna hatari ya kuvuja kwa taarifa za ndege hiyo isiyo na rubani.
Kabla ya hapo msemaji wa jeshi la Kizayuni alikuwa ametangaza habari ya kutunguliwa ndege nyingine isiyo na rubani ya utawala huo katika anga ya Syria.
Inavyoelekea ni kuwa hivi sasa ndege zisizo na rubani za Israel zinatunguliwa mara kwa mara nchini Syria zaidi ya huko nyuma. Hivyo inaonekena kwamba Syria iko tayari kutoa pigo kwa utawala wa Kizayuni.
342/