Uingereza ilijiondoa rasmi katika Umoja wa Ulaya Januari 31, 2020 baada ya kura ya maoni iliyofanyika mwaka 2016 ya kuamua kujitoa au kubaki katika umoja huo.Kwa mujibu wa shirika la habari la ISNA, matokeo ya uchunguzi wa maoni uliofanywa na taasisi ya YouGov yaliyotolewa jana Jumanne yalionyesha kuwa 57% ya Waingereza wanahisi Brexit ni tukio lisilo sahihi. Kulingana na watu hao, Brexit haijaleta taathira yoyote chanya ya kiuchumi kwa nchi hiyo.
Kwa upande mwingine, 32% ya walioshiriki kutoka maoni yao wamesema wanaamini Brexit ilikuwa hatua sahihi. Asilimia 55 ya waliohojiwa wamesema iwapo kura ya maoni kuhusu Brexit itarudiwa, watapiga kura nchi yao ibaki katika Umoja wa Ulaya, huku asilimia 31 wakisema watapiga kura ya kujiondoa tena katika Umoja wa Ulaya. 63% ya watu waliotoa maoni yao katika uchunguzi huo wa maoni uliofanywa na taasisi yaYouGov sasa hivi wanaichukulia zaidi Brexit kama uamuzi wa kufeli na kuharibikiwa kuliko kuwa wa mafanikio kwa Uingereza. Utafiti wa YuGov umeonyesha pia kuwa ni 12% tu ya waliohojiwa wamesema kujiondoa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya ilikuwa hatua ya mafanikio, huku18% wakisema hatua hiyo haikuwa ni mafanikio wala ya kufeli. Mnamo mwezi Mei, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak alidai kuwa Brexit imeleta manufaa ya kiuchumi kwa nchi hiyo.../
342/