Katika mapigano yaliyotokea jana Jumanne mjini Nablus, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel waliwaua shahidi Wapalestina watatu na kupeleka miili yao sehemu isiyojulikana.
Mapigano hayo yalitokea katika kituo cha usalama cha utawala wa Kizayuni karibu na Mlima Gerizim huko Nablus.
Akihutubia wananchi wa Palestina na makundi ya mapambano ya ukombozi, Nasser Kan'ani ameongeza kuwa: "Damu safi ya mashahidi wenu haitapotea bure na utawala bandia, vamizi na wa kigaidi wa Israel unakaribia kuangamia."
Jumatatu wiki hii wakati wa kuidhinishwa mageuzi ya mahakama katika Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel, Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon aliitaja siku hiyo kuwa siku mbaya zaidi kwa utawala huo na kusema: Matukio hayo yatawaangamiza Wazayuni.
342/