Ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X Jumapili kuwa hali ya kibinadamu huko Gaza ni mbaya na kila dakika inazidi kuwa mbaya.Sanders ameongeza kuwa Israel lazima iheshimu sheria za kimataifa na kuruhusu wanaume, wanawake na watoto wasio na hatia kupata chakula, maji, vifaa vya matibabu na mafuta. Seneta huyo wa Marekani amekitaja kitendo cha kinyama cha utawala wa Israel cha kuishambulia kwa mabomu hospitali ya Al-Maamadani kaskazini mwa Gaza kuwa ni jinai isiyoelezeka.
Katika taarifa hiyo, Sanders amesisitiza kwamba mabomu na makombora yanayotumiwa na utawala wa kigaidi wa Israel dhidi ya raia yanapaswa kukomeshwa haraka iwezekanavyo, misaada ya kibinadamu kutumwa Gaza ili kukidhi mahitaji ya raia, na kuwa mateka wa Marekani wanapaswa kurejeshwa kwa familia zao haraka iwezekanavyo.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa na Wizara ya Afya ya Palestina, idadi ya mashahidi wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni Gaza imefikia zaidi ya watu elfu nane, ambapo watu elfu tatu na laki tatu na ishirini na wanne ni watoto, elfu mbili sitini na mbili ni wanawake na 460 ni wazee.Takwimu hizo zimetangazwa katika siku ya 23 ya vita dhidi ya Gaza, wakati ambapo ndege za kivita za Israel zinaendelea kushambulia kwa mabomu maeneo ya raia ya ukanda huo.
Ashraf al-Qadara, Msemaji wa Wizara ya Afya ya Gaza amesema: Utawala wa Kizayuni umefanya mauaji 56 masaa machache yaliyopita, na matokeo yake ni kuwa watu 302, wengi wao wakiwa ni watu waliokimbilia usalama wao kusini mwa Ukanda wa Gaza, wameuawa shahidi.
342/