Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA imesema hospitali za Shifa na Al Quds katika mji wa Gaza na hospitali ya Indonesia kaskazini mwa Gaza, zimeshambuliwa mwishoni mwa juma.
Shirika hilo limeongeza kuu hujuma hizo ziliifuatia wito uliotolewa upya na jeshi la katili la Israel la wagonjwa kuondoka katika vituo hivyo vya afya mara moja.
Kwa mujibu wa OCHA, takriban watu 117,000 waliokimbia makazi yao wanahifadhiwa katika hospitali 10 ambazo bado zinafanya kazi katika mji wa Gaza na mahali pengine kaskazini mwa Gaza, ambazo zimepokea maagizo ya kurejewa kwa wito wa kuondoka katika siku za hivi karibuni.
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO kupitia ukurasa wake a X lnalo imesema "kuhamishwa kwa hospitali nzima haiwezekani bila kuhatarisha maisha ya wagonjwa".Kwa upande wake shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi duniani UNFPA limesema hali ni mbaya sana hasa kwa kina mama wanaojifungua kwani hivi sasa upasuaji wa wanawake kujifungua unafanywa bila ganzi huku kukiwa na uhaba mkubwa wa vifaa vya matibabu na nishati, na wakati mwingine madaktari wanabidi kuzalisha watoto njiti wa kina mama wanaofariki dunia.”
Hayo yanajiri wakati ambao, Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza imetangaza kuwa, hadi kufikia jioni ya Jumatatu idadi ya Mashahidi wa mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo imeongezeka na kufikia watu 8,306.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hii, watu 21,048 wamejeruhiwa kwa viwango tofauti na kwamba waliouawa shahidi 3,457 ni watoto na 2,136 ni wanawake.
342/