Vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya ukanda wa Gaza vimefikia hatua nyeti katika anga ya ndani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za palestina (Israel). Mzozo kati ya wanajeshi na wanasiasa ndani ya Baraza la Mawaziri la Netanyahu, pamoja na mvutano ndani ya baraza la mawaziri la vita, imejitokeza hadharani na haifichiki tena. Yoav Gallant, Waziri wa Vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel anampinga waziwazi Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu, hali inayoashiria kutoaminiana zaidi pande hizo mbili ikilinganishwa na hapo awali. Tangu mwanzoni mwa vita vya Gaza, Netanyahu na Gallant walikuwa na tofauti za kimbinu na kimitazamo kuhusu usimamizi wa vita, lakini tofauti hizi zilikuwa za siri na zilidhihiri zaidi katika uhusiano pande mbili tu. Hivi sasa tofauti hizo sio siri tena na zimefika katika vikao vya baraza la vita kuhusiana na matukio ya Gaza. Ripoti zinasema kuwa Netanyahu na Yoav Gallant huzungumza mara chache sana. Vilevile inasemekana kuwa, Waziri Mkuu wa utawala ghasibu wa Israel ana wasiwasi kuhusu mashauriano ya siri ya Gallant na maafisa wa Ikulu ya White House na hata baadhi ya wapinzani wake katika shirika la ujasusi la Mossad. Inaonekana kuwa Netanyahu hana imani tena na waziri wake wa vita.Upande mwingine wa pengo hili umeonekana ndani ya baraza la mawaziri la vita. Gadi Eisenkot, mmoja wa wajumbe wakuu wa baraza la mawaziri la vita la utawala wa Kizayuni alimshutumu Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu katili, kuwa hakuweka bayana malengo ya kijeshi ya Israel huko Ukanda wa Gaza. Eisenkot ambaye ametaka kufanyike uchaguzi mpya huko Israel, amesema kwamba wale wanaounga mkono fikra ya kuangamizwa kikamilifu harakati ya Hamas hawasemi ukweli.
Kauli hii ya Eisenkot imetolewa katika hali ambayo kabla ya kumalizika miezi mwili ya vita vya Gaza, yeye na baadhi ya maafisa wa Kizayuni walidai kwamba inawezekkana kuliangamiza kundi la Hamas, na kuwa Netanyahu hakuwa akibabaisha kuhusiana na suala hilo. Hata hivyo kutofikiwa malengo hayo ya waziri mpenda vita na muuaji wa watoto wa utawala haramu wa Israel hakujaacha nafasi ya kumtetea, hata kwa wapambe wake wa karibu kama Gadi Eisenkot. Wakati huo huo, Benny Gantz, mjumbe mwingine wa baraza la mawaziri la vita, ameleza waziwazi tofauti zake na Netanyahu na alishiriki katika maandamano dhidi yake na kutaka rasmi aondolewe madarakani.Tofauti hizo zimemweka Netanyahu katika hali kugumu. Hivi sasa bunge la utawala wa Kizayuni linachunguza suala la kumuuuzulu waziri mkuu katika hali ambayo serikali ya Tel Aviv iko katika vita na inakabiliwa na hali mbaya katika mapigano ya Gaza. Ingawa ni jambo lililo mbali kuuzuliwa Netanyahu kupitia njia ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye bungeni katika kipindi kifupi lakini jambo hilo linaweza kuwa mwanzo wa kumalizika maisha ya kisiasa ya chinjachinja huyo wa watu wa Gaza na washirika wake. Mchakato wa kura ya kutokuwa na imani na Netanyahu unahitaji angalau kura 61 za wanachama wa Knesset, wakati muungano wa serikali ya Netanyahu una wingi wa viti 64. Hata hivyo, baadhi ya wanachama wa chama cha Likud wamemtema Netanyahu na wanataka aondolewe katika nafasi ya uwaziri mkuu. Inaonekana kwamba suala hilo ni kengele ya hatari ya kwa baraza la mawaziri la Netanyahu. Kwa mujibu wa matokeo ya uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni, muungano unaoongozwa na Netanyahu utashindwa iwapo uchaguzi wa mapema wa bunge utafanyika, na muungano wa upinzani utapata kura zinazohitajika. Uchunguzi huo wa maoni umeonyesha kuwa Benny Gantz, waziri wa zamani wa vita na mjumbe wa sasa wa baraza la mawaziri la vita la Israel, ana nafasi nzuri zaidi ya kuchukua kiti cha uwaziri mkuu.
342/