Sayyid Hassan Nasrullah ameyasema hayo katika hotuba aliyoitoa katika mji mkuu wa Lebanon Beirut kwa mnasaba wa kumuenzi Shahid Sayyid Ebrahim Raisi na wenzake waliokufa shahidi pamoja naye katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili iliyopita kaskazini magharibi mwa Iran. Nasrullah vilevile amemtaja Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian, ambaye naye pia alikufa shahidi katika tukio hilo kuwa ni "muumini wa Muqawama na harakati zake." Katibu Mkuu wa Hizbullah amesema, tukio hilo la msiba "limeumiza sana na kuhuzunisha sana ndani ya Iran na nje ya nchi." Aidha, ameashiria jinsi mazishi ya mashahidi hao yalivyohudhuriwa na mamilioni ya watu katika Jamhuri ya Kiislamu na kusema: "shughuli hiyo ya mazishi ilikuwa ya tatu kwa ukubwa katika historia ya wanadamu baada ya Imam Khomeini na Shahidi Qassem Soleimani". Sayyid Hassan Nasrullah alieleza hayo kuashiria mazishi ya Hayati Muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu na ya Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC).Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Katibu Mkuu wa Hizbullah amezungumzia vita vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni mwezi Oktoba na kuendelea hadi sasa dhidi ya Ukanda wa Ghaza kufuatia operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya kulipiza kisasi iliyofanywa na harakati za Muqawama za Ghaza na akasema, adui anakiri kuhusu mateso makali anayopata, anakubali kuwa ni dhaifu na kwamba ameshindwa kufikia malengo yake.
Sayyid Hassan Nasrullah amesema, leo tukiwa katika mwezi wa nane wa vita dhidi ya Ghaza, Waisraeli wenyewe walioko madarakani na wapinzani, wote wanakubali kwamba unayokabiliana nayo utawala huo hivi sasa haujawahi kuyashuhudia.
Vile vile amesisitiza kuwa iwapo utawala haramu wa Israel utaendelea na vita "utaingia shimoni," na kuonya kwamba makundi ya Muqawama yameweka akiba ya mambo ya "kushangaza" kwa ajili ya utawala huo.
Amemhutubu Netanyahu kwa kumwambia: "inakupasa utarajie ya kushangaza kutoka kwa Muqawama wetu".../
342/