BJP iliibuka kirahisi kama chama kikubwa zaidi kitaifa katika Lok Sabha, bunge la chini la India. Wakati wasimamizi wa uchaguzi nchini India walihesabu kura milioni 640 ndani ya siku moja Jumanne, baada ya uchaguzi uliochukua wiki sita, BJP ilipata hasara kubwa ikilinganishwa na ushindi wake katika miaka ya 2014 na 2019.
Tofauti na chaguzi zote mbili ambapo BJP ilishinda wingi wa viti kivyake, mara iliishia kupata viti 240 katika bunge hilo lenye viti 543, wakati idadi iliyohitajika ili kupata wingi mutlaki ni viti 272.
Kinyume chake, muungano wa upinzani wa Indian National Developmental, Inclusive Alliance kwa kifupi INDIA, unaoongozwa na chama cha Congress, ulishinda viti 223, ikiwa ni zaidi ya ilivyotabiriwa.
Modi na chama chake bado wana uwezekano wa kuunda serikali ijayo ya India - lakini itategemea kundi la washirika ambao itawahitajia ili kupata viti zaidi ya 272. BJP na washirika wake, katika muungano unaojulikana kama National Democratic Alliance (NDA), wameshinda jumla ya viti 283.
Katika muongo mmoja uliopita chini ya serikali ya BJP, India imeteleza kwenye fahirisi kadhaa za kidemokrasia huku kukiwa na shutuma za kuwakandamiza wapinzani, Waislamu na vyombo vya habari.
342/