Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars; Erdogan alisema hayo jana (Jumapili) na kuongeza kwamba wamekusudia kwa dhati kumwalika Rais Bashar al Assad kutembelea Uturuki karibuni hivi.
Shirika la habari la Anadolu limeripoti habari hiyo na kumnukuu Edrogan akisema pia kwamba: "Tunatumai tutaweza kurudisha uhusiano wa Uturuki na Syria kama ulivyokuwa siku za nyuma."
Vile vile amesema: "Tunachakizungumzia hapa ni upatanishi. Kwa nini tusikubali suluhu? Tunaweza kuwaalika Bw. Assad na Bw. Putin watembelee Uturuki."
Katika miaka ya hivi karibuni, na licha ya kupungua mivutano kati ya serikali nyingi za eneo hili na Syria, lakini uhusiano wa Ankara-Damascus haujarudi kama ulivyokuwa zamani. Kwa mtazamo wa serikali ya Syria, kikwazo kikubwa ni uungaji mkono wa Uturuki kwa magenge ya kigaidi yanayofanya mauaji dhidi ya raia na maafisa wa serikali nchini Syria kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.
Serikali ya Syria imekuwa ikitangaza mara kwa mara kuwa Uturuki inapaswa kukomesha kuzikalia kwa mabavu ardhi ya Syria na kuacha kuunga mkono magenge ya kigaidi. Damascus inasisitiza kuwa "Makubaliano ya Adana" (1998) ndiyo makubaliano bora zaidi ya kutatua masuala yaliyopo kati ya Syria na Uturuki.
Amma kuhusu Palestina, Rais wa Uturuki amegusia mazungumzo yasiyo rasmi kati ya mkuu wa Mossad na maafisa wa Hamas mjini Doha Qatar na kusema kuwa hatua nzuri zimechukuliwa ambazo zinaweza kushuhudia usitishaji wa kudumu wa mapigano huko Ghaza.
342/