13 Agosti 2024 - 12:44
Dkt. Sahar Mustafa: Kuhudhuria Matembezi ya Arbaeen ni kutoa (Bai'a) kiapo cha utii kwa Imam Hussein (a.s)

Profesa wa Chuo Kikuu cha Lebanon alisema: Kuhudhuria Arbaeen ni kutoa (Bai'a) kiapo cha utii kwa Imam Hussein (a.s) na ni kujifunza maadili ya Kibinadamu ambayo alituletea Yeye pamoja na Hazrat Zainab (Amani iwe juu yao).

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Madam Dkt. Sahar Mustafa, ambaye ni mmoja wa walimu wa Hawzat na Chuo Kikuu nchini Lebanon, alisema katika mtandao wa kwanza wa Kimataifa "The Global Message of Arbaeen of Hussein" kwamba Arbaeen ya Hussein inaweza kutuonyesha Maadili ya Kibinadamu na yenye kuhitajika Kifamilia.

Aliongeza: "Tunaweza kujifunza maadili ya Ujasiri (Ushujaa), Haki na Subira kutoka ndani ya Arbaeen ya Imam Hussein (as). Maadili ambayo Hazrat Zainab (s.a) aliweza kutuletea kutokana na uwepo wake (katika ardhi ya Karbala).

Profesa huyo wa Chuo Kikuu cha Lebanon aliongeza kusema:

Kuhudhuria Matembezi ya Arbaeen ya Imam Hussein (a.s) ni kutoa (Bai'a) kiapo cha utii kwa Imam Hussein (a.s) na ni kujifunza Maadili ya Kibinadamu ambayo yeye na Hadhrat Zainab (s.a) walituletea.

Dkt. Sahar Murtaza alisema: Vijana hawapaswi kuwa hasi. Arbaeen inaweza kuwaelimisha vijana kwa njia chanya. Jukumu la familia huko (katika Matembezi ya) Arbaeen ni mojawapo ya vipengele bora kabisa vya Maadili ya Kibinadamu.