Maulid hii imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa kama ifuatavyo:
1_Mke wa Balozi wa Iran Nchini Tanzania.
Ambaye alimuongelea kwa undani zaidi Mtume Muhammad (s.a.w.w), na ifuatayo ilikuwa maudhui ya mada yake:
"MJUE MTUME MUHAMMAD (S.A.W.W); TABIA NZURI NA MAADILI MEMA ALIYOYALETA DUNIANI"
2_Mama Shamim Khan, Mwenyekiti wa JUWAKITA Kitaifa.
Katika Hotuba yake aliongelea juu ya:
UMUHIMU WA MWANAMKE KATIKA UISLAMU NA ELIMU KWA MWANAMKE WA KIISLAMU.
Mada nyingine katika Mnasaba huu iliwasilishwa na Mwenyekiti wa Wanawake wa T.I.C _ TAIFA, Ukhti Fatima Mwiru, ambapo aliongelea juu ya:
JUKUMU LA MWANAMKE KATIKA NYANJA ZOTE ZA MAISHA.
Alibainisha kwamba: Wanawake ni sehemu muhimu ya jamii. Wanawake ni nusu ya idadi ya watu duniani, na wao ndio jiwe la msingi wa maendeleo endelevu katika jamii yoyote Duniani.
Mwanamke ndiye anayewajibika hasa katika kuamua aina ya maisha ambayo familia watayaishi.
Kuna Majukumu tofauti tofauti ambayo Mwanamke huyasimamia katika jamii, kama vile:
1_Majukumu ya Mwanamke kama Mama.
2_Majukumu ya Mwanamke kama mke.
3_Majukumu ya Mwanamke kama Kiongozi.
4_Majukumu yake kama afisa.
5_Majukumu yake kama Dada.
6_Majukumu yake kama rafiki.
Na Majukumu mengine muhimu zaidi ya Wanawake wenye athari kubwa katika ujenzi wa Jamii za Wanadamu.