13 Oktoba 2024 - 18:20
Imamu wa Swala ya Ijumaa wa Najaf Al-Ashraf: Ayatollah "Sistani "Ni ishara ya Amani na Ubinadamu”

Hojjat-ul-Islami wal Muslimina, "Syed Sadruddin Qabanchi" alisema: Israel ilimlenga Ayatollah Sistani kwa ajili ya kumuua kigaidi; huku ikijua kuwa Shakhsia hii inapandisha (inanyanyua juu) Bendera ya Amani na Ubinadamu.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Hojjatul Islami wal Muslimina, "Syed Sadruddin Qabanchi", Imamu wa Ijumaa wa Najaf al-Ashraf, alisema katika khutba za Swala ya Ijumaa alizozitoa katika Husseiniyyah Tukufu ya Fatemiyyah, Najaf al-Ashraf: Tunashuhudia kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa “dhoruba ya Al-Aqsa” iliyotokea mnamo Oktoba 7 mwaka jana, wakati Israeli ilipoamua kuiangamiza kabisa Gaza, na kwa kweli ilianza kushambulia kwa mabomu, kuharibu majumba na kisha kusonga mbele ardhini.

Akaongeza kusema: Hivi sasa tuko katika mwaka wa pili wa Dhoruba ya Al-Aqsa, ambapo idadi ya mashahidi imefikia 41,000, na matokeo yake ni kama ifuatavyo:

Kwanza: Israel haiwezi kuangamiza Muqawamah (Upinzani) wa Gaza. Pili: Kushindwa kwa jamii ya Kimataifa katika kuharibu Muqawamah. Tatu: Kuongezeka kwa mwamko wa Kiislamu na Kimataifa dhidi ya Israel. Nne: Mifarakano na hitilafu ndani ya utawala wa Kizayuni. Tano: Kuondolewa kwa Barakoa (Mask) ya Ulimwengu wa Magharibi na madai yao ya Haki za Binadamu na Uhuru wa Mataifa. Sita: Kuingia kwa Iran, Iraq, Lebanon na Yemen katika mstari wa mbele wa mapambano ya Upinzani (Muqawamah). Saba: Kuongezeka kwa mhimili wa Upinzani (Muqawamah). Nane: Ni kwamba mipigo ya Iran yamethibitisha kuwa Israel ni nyumba ya vioo.

Kuhusu Ayatollah Sistani, Hojjat-ul-Islami wal-Muslimina Qabanchi alisema: Israel ilimlenga Ayatollah Sistani kwa ajili ya kumuua kigaidi, huku ikijua kwamba mtu huyu ni mshika bendera wa amani na ubinadamu.

Imam wa swala ya Ijumaa wa Najaf al-Ashraf ameongeza kuwa: Suala hili linaonyesha kuwa Israel ni kundi la kigaidi, nasi tukiwa tunaendelea na kukilaani kitendo hiki (kitisho cha Israel kwa Ayatollah Sistani), tunauonya utawala dhalimu wa kizayuni juu ya uvamizi wowote dhidi ya Iraq, kwa sababu hilo linaiweka rasmi Iraq katika mstari mbele wa Upinzani (Muqawamah).