5 Novemba 2024 - 12:31
Marekani imemuomba Kiongozi wa Iran asijibu uchokozi wa Israel

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwa mara nyingine tena ameitaka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kutojibu mashambulizi ya hivi karibuni ya utawala wa Kizayuni katika ardhi ya Iran.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul_Bayt (a.s) - ABNA - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani "Matthew Miller" aliitaka Jamhuri ya Kiislamu kwa mara nyingine tena wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari siku ya Jumatatu kutojibu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni (yaliyofanyika) katika baadhi ya maeneo ya Iran.

Kwa mujibu wa ripoti ya tovuti ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ililiripoti kuhusu matamshi ya hivi karibuni ya Ayatollah Khamenei kwamba "maadui, kwa ujumla Marekani na utawala wa Kizayuni", wanapaswa kujua kwamba bila shaka watapata jibu kali kwa kile wanachokifanya dhidi ya Iran na upande wa Safu ya Upinzani (Muqawamah)."

Aliuliza swali, ambalo "Miller" alilitolea ufafanuzi akijibu kwamba:

"Ujumbe wetu kwa Kiongozi Mkuu ni ujumbe ule ule mliousikia wiki iliyopita, na ni huu kwamba hapaswi kujibu / kulipiza zaidi."

Hapaswi kuzidisha zaidi hali hii ya sasa, na akichagua chaguo kama hilo, tutaisaidia Israel kujilinda yenyewe."

Tangu kuanza kwa shambulizi la mapema asubuhi la utawala haram wa Kizayuni katika baadhi ya maeneo ya Iran, waitifaki wa utawala wa Kizayuni hususan Marekani wameitaka Iran kujizuia na kutojibu mashambulizi hayo.

Hata hivyo, Tehran imesisitiza kuwa bila shaka itatoa jibu la uhakika kwa hatua hiyo ya utawala haram wa Kizayuni.

Kuhusiana na hilo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema:

Kile ambacho utawala wa Kizayuni ulikifanya tarehe 27, October 2024 ni shambulio jipya dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema kwamba:

Imepelekea kutupa kwa mara nyingine tena haki mpya ya kujibu shambulio hilo kwa anuani ya Haki ya kujihami (na kujilinda), na pia imeshatangazwa kuwa hilo litafanywa".