21 Desemba 2024 - 15:54
Mkutano "Uwezeshaji kamili wa Wanawake kwa kumuiga Hazrat Zahra (s.a)" ulifanyika nchini Zimbabwe + Picha

Sambamba na Siku ya Kuzaliwa kwa Hazrat Zahra (s.a), mkutano wa kina mama wa uwezeshaji wa Wanawake kwa kumuiga Sayyidat Fatima Zahra (s.a) ulifanyika nchini Zimbabwe.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Sambamba na Siku za kuzaliwa kwa Hazrat Zahra (amani iwe juu yake), mkutano wa uwezeshaji wa kina mama (Wanawake) kupitia kumuiga Hazrat Zahra (s.a) katika Maendeleo ya kiroho, kijamii na kiakili kwa Wanawake ulifanyika katika Taasisi ya Imam Hussain (s.a) nchini Zimbabwe.

Katika hafla hii, wazungumzaji mashuhuri wa Jumuiya ya Wanawake ya Zimbabwe, Bi. Taybeh Balakazi, Tersha Mosenzi, Tende Zahra Louise na Bi. Dk. Rebecca Masterton kutoka Uingereza, waliwasilisha maoni yao kwa njia ya mtandaoni.