Netanyahu alidai: Sasa tuko katika hatua mbaya na mfululizo wa mashambulizi tuliyofanya yamebadilisha sura ya Mashariki ya Kati.
Maneno hayo ya Netanyahu yameelezwa saa chache baada ya duru za Kizayuni kudai kuwa mazungumzo ya kubadilishana wafungwa na harakati ya Hamas yapo kwenye mkondo sahihi na kwamba orodha ya majina ya wafungwa wa Kipalestina ya kubadilishana na wenzao wa Israel imeandaliwa katika hatua ya kwanza ya kubadilishana wafungwa kati ya pande hizo mbili.