31 Desemba 2024 - 04:08
Mkutano "Jukumu la familia katika uundaji wa Shule ya Suleimani" ulifanyika nchini Nigeria

Mkutano wa "Jukumu la familia katika uundaji wa Shule ya Suleimani" uliandaliwa na ushauri wa Kitamaduni wa Iran nchini Nigeria.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - ABNA - Mshauri wa Masuala ya Kiutamaduni ya Iran nchini Nigeria, katika mkesha wa mwaka wa tano wa kuuawa Shahidi Hajj Qassem Suleimani, ameandaa mfululizo wa programu na mikutano maalumu kuhusiana na maelezo ya mitizamo na fikra za Shahidi huyo wa ngazi ya juu katika uwanja wa Uislamu, Mapinduzi na Upinzani (Muqawamah), pamoja na maisha yake kuhuisha kumbukumbu ya kiongozi huyo wa Upinzani (Muqawamah) ndani ya nyoyo zetu na kumtambulisha kama ishara ya ujasiri, muhanga, ushujaa na amani kwa jumuiya ya kimataifa.

Kuhusiana na hili, alifanya mkutano wa kwanza unaozingatia nafasi ya familia chini ya anuani hii: "Jukumu la Familia katika Uundaji wa Shule ya Suleimani" nchini Nigeria.