Shirika la habari la Anadolu la Uturuki limeripoti habari hiyo na kueleza kuwa, maandamano hayo yalifanyika jana Ijumaa mbele ya jengo la Tume ya Ulaya, kabla ya mkutano ujao wa Baraza la Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na Israel uliopangwa kufanyika Jumatatu ijayo.
Waandamanaji hao walikuwa na mabango yenye ujumbe unaoitaka EU kuunga mkono amani na haki kwa watu wa Palestina, na kukomesha uvamizi wa Israel.
John Doyle, mfanyakazi wa Umoja wa Ulaya, ameiambia Anadolu kwamba, walikusanyika ili kuonyesha mshikamano na watu wa Gaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan, na Lebanon dhidi ya utawala wa Israel.
Hapo awali, karibu wafanyakazi 200 wa Umoja wa Ulaya pia walikuwa wamefanya mazishi ya mfano nje ya majengo ya Tume na Baraza la Ulaya kuomboleza kifo cha sheria za kimataifa, mikataba ya EU, Mkataba wa Mauaji ya Kimbari, na maadili ya Ulaya.
Hali kadhalika, wafanyakazihao wa Umoja wa Ulaya walikaa kimya kwa dakika moja kuwakumbuka na kuwaenzi Wapalestina waliouawa huko Gaza.
342/