Katika ujumbe kupitia ukurasa wake kwenye X, Sheikh Ahmed bin Hamad Al Khalili amelezea hali mbaya ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza na kusisitiza umuhimu wa kuwasaidia watu wanaodhulumiwa katika eneo hilo la Wapalestina.
Kwa mujibu wa ripoti ya jarida la Al-Arabi al-Jadid, amesema kuna haja ya mshikamano na msaada kwa watu wa Palestina, akiongeza kuwa jinsi ambavyo watu huunga mkono familia na jamaa zao wanapopitia magumu, wana wajibu wa kusimama pamoja na watu wa Gaza.
Akitilia mkazo umuhimu wa misaada ya kibinadamu, ameongeza, "Tunawahimiza watu wote wenye huruma na mioyo ya upendo duniani kote kutilia maanani hali mbaya ya Gaza na kuchukua hatua za kuwasaidia, kwani athari za hisani daima huwa za milele na hudumu kwa muda mrefu."
Kwingineko katika ujumbe wake huo, Mufti Mkuu wa Oman amesifu msimamo thabiti wa wapiganaji wa muqawama wa Yemen dhidi ya utawala wa Israel na kuuelezea kama majibu ya haki kwa uhalifu wa Wazayuni.
Ijumaa, kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen, Abdul Malik Badreddin al-Houthi, aliupa utawala haramu wa Israel muhula wa siku nne kuhakikisha misaada ya kibinadamu inaingia Gaza, akionya kuwa vinginevyo, mashambulizi ya kijeshi ya Yemen dhidi ya malengo ya Israel yangeanza tena.
Baada ya kuanza jinai ya mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Wapalestina wa Gaza mnamo Okotoba 2023, Jeshi la Yemen lilianza kushambulia meli za Israel na meli zinazobeba shehena kuelekea katika bandari zinazokaliwa kwa mabavu na Israel ambazo zilikuwa zikipita katika Bahari ya Sham.
Operesheni hizo zilileta athari kubwa kwa uchumi wa Israel, na kusababisha kupanda kwa bei ya bidhaa mbalimbali zinazotumiwa na walowezi wa utawala huo haramu.
342/
Your Comment