Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahl al-Bayt (A.S) - Abna -: Seneta Raja Nasser Abbas Jafari, Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan, katika taarifa yake amelaani mauaji ya Mufti Munir Shakir, Mwanazuoni wa Kisunni wa Pakistan, na kuyataja kuwa ni hasara isiyoweza kufidiwa.
Aliongeza: Ninalaani vikali shambulio hili la kigaidi la woga, ambalo ni thibitisho la hofu ya watu wenye msimamo mkali kutoka kwa wahubiri hao shupavu na wasio na woga ambao waliwasha Mshumaa wa Umoja, Udugu na Ukweli.
Raja Nasser aliendelea kusema: Mufti Munir Shakir alikuwa mmoja wa watetezi wakubwa wa Umoja miongoni mwa Waislamu ambaye alijitolea maisha yake katika kukuza na kuimarisha Umoja, Udugu na Amani miongoni mwa Umma (wa Waislamu).
Mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Waislamu wa Pakistan amesema kuwa, kuuawa Shahidi Mufti Munir Shakir ni hasara kubwa, na akaongeza: Ninaiomba sana Serikali ya sasa kwamba wahusika waliohusika na jinai hiyo ya kinyama wapelekwe mbele ya haki haraka iwezekanavyo na kwamba uungaji mkono wa Wanazuoni na Wahubiri hao wenye msimamo imara na ambao ni Mashujaa wa Udugu, Upendo na Maelewano uhakikishwe kwa gharama yoyote ile. Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema Peponi Mufti Munir Shakir na awape subira familia na jamaa zake.
Your Comment