19 Machi 2025 - 14:06
Takriban Maafisa watano wa ngazi za juu wa Hamas wameuawa Shahidi katika Mashambulizi ya anga ya Israel huko Gaza

Takriban maafisa watano wa ngazi za juu wa Hamas wameuawa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya anga ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la AhlulBayt (a.s) - ABNA -; Takriban maafisa watano wa ngazi za juu wa Hamas wameuawa katika mashambulizi ya hivi karibuni ya anga ya Israel kwenye Ukanda wa Gaza. 

Miongoni mwa Maafisa hao waliouliwa ni pamoja na Mohammad Al-Jmasi, Mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa, na watu kadhaa wa familia yake, wakiwemo wajukuu zake. Sputnik iliripoti.

Walikuwa ndani ya nyumba yake katika Mji wa Gaza wakati ilipopigwa katika shambulio la anga. Hii ni kulingana na vyanzo vya Hamas na jamaa zake kama ilivyotajwa na Reuters.

Mahmoud Abu Watfa, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Hamas, ambaye alisimamia Jeshi la Polisi la Hamas, na Issam Aldialis, Kamanda wa usalama wa ndani, pia walikuwa miongoni mwa waliouawa Shahidi, Ynet iliandika.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha