19 Machi 2025 - 16:15
Wakimbizi wapya 13,000 wa Syria wamekimbilia Lebanon / wakikimbia uhalifu wa Al-Julani kwenye Pwani ya Syria

Takriban wakimbizi wapya elfu 13 wa Syria wameingia katika vijiji na miji 23 Kaskazini mwa Lebanon.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (AS) - Abna -; Baraza la Kusimamia Migogoro na Maafa (Majanga) la Mkoa wa Akar ilitangaza katika ripoti yake kwamba takriban wakimbizi wapya 13,000 wa Syria wamepatiwa hifadhi tangu kuanza kwa mizozo katika eneo la Sahel Magharibi mwa Syria, mnamo Machi 6 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti hii, Wasyria 12,789 waliingia katika majimbo ya mpakani ya Lebanon, na watu hawa waliokimbia makazi yao walikaa katika miji na vijiji 23 wakiwa na familia zao au katika kumbi mbalimbali na maghala.

Baraza la Kukabiliana na Migogoro na Majanga lilitangaza kwamba ongezeko kubwa la kuwasili kwa wakimbizi wa Syria katika vijiji vya eneo la Sahl Akar na maeneo ya mpaka kati ya Lebanon na Syria kumezua changamoto nyingi katika uwanja wa utoaji wa malazi, chakula na huduma za kimsingi za afya katika kivuli cha uwezo mdogo wa manispaa na jamii zinazowapokea.

Eneo la Sahel nchini Syria limeshuhudia vitendo vya ukatili kwa siku kadhaa tangu Machi 6 mwaka huu. Kwa kisingizio cha kukabiliana na waasi wanaomuunga mkono Bashar al-Assad, Serikali ya Julani ilituma vikosi vya kijeshi katika maeneo ya Waalawi, na kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Haki za Binadamu la Syria, vikosi vya (kigaidi) vya Julani vilifanya jinai na mauaji ya wazi uwanjani, na vitendo vya maafisa wa Serikali ya Kigaidi ya Julani vilisababisha vifo vya raia 1,500, wengi wao wakiwa Wa_Alawi.

Shirika la Kuchunguza Haki za Binadamu la Syria lilitangaza kuwa tangu kuanguka kwa Serikali ya Bashar al-Assad tarehe 8 Disemba mwaka jana, raia 4,711 wameuawa nchini Syria. Kulingana na ripoti hii, raia 1805 waliuawa kwa njia ya kunyongwa mashambani. Wakati huo huo, familia yote ikiwa ni pamoja na Wanawake, Watoto na Wazee waliuawa kabisa (na kutoweshwa kiujumla). Watu wenye silaha pia walishambulia nyumba za watu na kuwauliza kama walikuwa Wa-Alawi au Sunni kabla ya kuwaua au kuwasamehe.

Watu hao wenye silaha walirekodi video za mauaji yao dhidi ya raia kwa kuwapiga risasi kwa karibu zaidi, na kufuatiwa na vipigo na matusi.

Maafisa wa Serikali ya Kigaidi ya Julani waliunda kamati ya kutafuta ukweli!, ambayo wanasema itakusanya na kupitia ushahidi na ripoti zote zilizopo kuhusu matukio ambayo yalitokea hasa Machi 6, 7, na 8.

Baada ya mauaji hayo, ambayo yalilaaniwa kimataifa, maelfu ya wakaazi wa Pwani ya Syria walitafuta hifadhi katika kambi ya jeshi la Urusi ya Hmeimim, huku mamia ya familia wakikimbilia Kaskazini mwa Lebanon, ambayo inapakana na Pwani ya Syria.

Kwa mujibu wa ripoti rasmi, Lebanon imepokea takribani wakimbizi milioni moja na nusu wa Syria, ambapo 755,426 walisajiliwa na Umoja wa Mataifa. Wakimbizi hawa walitafuta hifadhi Lebanon wakati wa miaka ya mgogoro wa Syria ulioanza mwaka 2011.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha