Pars Today imeinukuu ISNA na kuripoti kuwa, kwa ushirikiano wa ubalozi mdogo wa Iran huko Guangzhou na Ofisi ya Mwambata wa Utamaduni mjini Beijing, kuanzia tarehe 21 hadi 26 Machi, Adnan Momineen, qaarii mashuhuri wa kimataifa kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekuwa akihudhuria ibada za mikesha ya Lailatul-Qadr katika mji huo sambamba na kusoma Qur'ani katika hafla hizo.
Moja ya ratiba na hafla za kisomo alizoshiriki Qaarii huyo kutoka Iran ni kusoma Qur'ani wakati wa Sala ya Ijumaa mjini Guangzhou katika Msikiti maarufu wa Abi Waqqas, hafla ambayo ilihudhuriwa na waumini zaidi ya 10,000 wa China, ambapo kisomo chenye mahadhi ya kuvutia cha Momineen kiliwasisimua sana Waislamu wa China.
Ratiba nyingine alizopangiwa Qaarii huyo kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kusoma kisomo cha Qur'ani katika Msikiti wa Haopen, Msikiti wa Guantalo, na katika Hussainiyyah ya Iran ya Wapenzi wa Ahlu-Baiti mjini Guangzhou.../
342/
Your Comment