26 Machi 2025 - 15:24
Source: Parstoday
HAMAS: Netanyahu anaongopa akidai vita vitawarejesha mateka wote wakiwa hai

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imemshutumu Waziri Mkuu wa Israel, Benjami Netanyahu kwa "kudanganya familia za [mateka], anapodai kuwa chaguo la kijeshi lina uwezo wa kuwarejesha (mateka wote) wakiwa hai."

HAMAS imesema katika taarifa kuwa, "Wakati wowote uvamizi huo unapojaribu kuwaokoa [mateka] wake kwa nguvu, huwarudisha wakiwa wamekufa kwenye majeneza." 

Imeongeza kuwa, kukiuka makubaliano ya kusitisha mapigano na kurejea vitani ni "uamuzi uliopangwa mapema" na Netanyahu, ambaye alisalimu amri mbele ya mashinikizo ya Waziri wa Usalama wa Kitaifa wa mrengo mkali wa kulia, Itamar Ben-Gvir.

Kundi hilo la Muqawama la Palestina limesema, "Netanyahu anabeba dhima kikamilifu kwa kufeli kwa makubaliano hayo, na jamii ya kimataifa na wapatanishi wanapaswa kumshinikiza kusitisha uchokozi na kurejea kwenye njia ya mazungumzo."

HAMAS: Netanyahu anaongopa akidai vita vitawarejesha mateka wote wakiwa hai

Kabla ya hapo, HAMAS ilitoa taarifa nyingine ikiwataka walimwengu wapinge uhalifu na mipango ya utawala wa Kizayuni dhidi ya ardhi ya Palestina, watu wake na maeneo yake matakatifu, na kulaani uungaji mkono wa Marekani kwa ukatili unaofanywa na utawala huo ghasibu.

Haya yanajiri huku Wapalestina 38 wakiuawa shahidi katika mashambulizi mapya ya Israel huko Gaza katika muda wa saa 24 zilizopita, kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya eneo hilo.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi Gaza imepindukia 800, tangu Israel ilipoanzisha upya vita vyake dhidi ya eneo lililozingirwa wiki iliyopita. Takriban Wapalestina 1,663 pia wamejeruhiwa kwenye hujuma hizo.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha