26 Machi 2025 - 15:27
Source: Parstoday
Takriban watu 1,400 wametiwa mbaroni huku maandamano yakiendelea Uturuki licha ya kupigwa marufuku

Mamlaha husika nchini Uturuki zimewatia mbaroni waandamanaji zaidi ya 1,400 huku maandamano ya mitaani yakiendelea kushuhudiwa katika miji mikubwa ya nchi hiyo kupinga marufuku ya kuandamana kufuatia kufungwa jela Meya wa mji wa Istanbul, Ekrem Imamoglu kwa tuhuma za ufisadi, kuongoza genge la uhalifu, utovu wa nidhamu na mengineyo.

Wananchi wa Uturuki wameandamana kwa usiku wa saba mtawalia hadi kufikia jana usiku wakipinga kuwekwa kizuizini Imamoglu, hasimu mkuu wa kisaisa wa Rais Recep Tayyip Erdogan.

Ali Yerlikaya Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki ametuma ujumbe katika mtandao wa X kwamba: Polisi ya Uturuki imewatia nguvuni watu 1,418 kwa kushiriki katika maandamano haramu na kuonya kuwa hakutakuwa na mjadala kwa wale wote wanaoibua ghasia mitaani.

Kwingineko, maelfu ya wananchi wa Uturuki jana katika usiku wa saba mtawalia waliandamana katika wilaya ya Sarachane makao makuu ya Istanbul City Hall ambako Imamoglu aligombea mwaka 2019, katika maandamano yaliyoitishwa na chama cha Wananchi wa Repuplican anachotokea.

Wakati huo huo Ozgur Ozel mkuu wa chama hicho ametoa wito wa kufanyika maandamano Jumamosi ijayo katika mji wa Istanbul akisema kuwa maandamano hayo yatakuwa kura ya maoni kubwa zaidi  ya wazi kuwahi kushuhudiwa katika historia na kwamba atashinikiza uchaguzi wa mapema ufanyike. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha