26 Machi 2025 - 15:27
Source: Parstoday
China yaitaka Syria iunde serikali shirikishi na ipambane na ugaidi

Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa amewataka viongozi wa mpito wa Syria waandae mchakato wa kuasisi serikali shirikishi na wachukua hatua madhubuti za kupabana na ugaidi nchini humo.

Fu Cong amesema katika kikao cha Baraza la Usalama la UN kwamba: Viongozi wa muda wa Syria wametangaza kuanza uchunguzi huru kwa muda wa mwezi mmoja kuhusu mauaji ya kiholela ya raia katika maeneo ya pwani ya nchi hiyo, mauaji ambayo yalikuwa kinyume cha sheria na ya kikatili. 

Cong ameongeza kuwa: China inafuatilia hatua zote zinaozchukuliwa kuhusu suala hilo na inataraji kuwa watawala wa mpito wa Syria watatekeleza majukumu yao kwa uwazi na kuwajibika. 

Mwakilishi wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa amesema: China imezingatia hatua za karibuni za viongozi wa muda wa Syria kwa ajili ya kufanikisha kipindi cha mpito cha kisiasa; na kuitaka serikali ya muda ya nchi hiyo itekeleze ahadi zake ipasavyo na kufanya mazungumzo na mashauriano na sekta zote za nchini Syria ili kujumuisha pande na makundi yote. 

Balozi wa China UN pia ameeleza wasiwasi wake kuhusu vitisho vipvya ya ugaidi huko Syria na kusisitiza udharura wa kudumishwa mapambano dhidi ya ugaidi.  

Fu amesisitiza kuwa mamlaka ya kujitawala, uhuru na umoja wa ardhi nzima ya Syria vinapasa kuheshimiwa na kulaani mashambulizi ya anga ya utawala wa Kzayuni dhidi ya Syria na kuutaka utawala wa Kizayuni uondoke haraka katika ardhi ya nchi hiyo.  

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha