Shirika la Kimataifa la Oxfam limesisitiza katika ripoti yake hiyo kwamba jamii ya kimataifa ni mshirika wa jinai za kivita za Israel huko Gaza kwa kusalia kimya na kutochukua hatua yoyote mkabala wa jinai hizo. Oxfam imetahadharisha kuwa, kuendelea mzingiro dhidi ya Gaza, kuzuiwa njia za kupitisha misaada, kuendelea kushambuliwa miundombinu na utoaji wa amri za kuwalazimisha watu kuhama katika eneo hilo si tu kwamba kumesababisha oparesheni za kibinadamu kusitishwa kwa kiasi kikubwa bali pia kumezidisha pakubwa hatari ya kuenea njaa kwa Wapalestina zaidi ya milioni moja.
Oxfam imebainisha katika ripoti yake kwamba: Tangu kuanza mshambulizi ya Israel tarehe 18 mwezi huu wa Machi dhidi ya Gaza yaliyokwenda sambamba na kushambuliwa pakubwa maeneo ya raia huko Jabalia na Khan Yunis; Wapalestina wasiopungua 700 wakiwemo watoto zaidi ya 200 wameuawa na wengine zaidi ya 120,000 wamelazimika kuhama makazi yao kufuatia kutolewa hukumu mpya ya kuhama kwa lazima katika hali ambayo hakuna sehemu yoyote ya Gaza iliyo salama.
Ripoti ya Shirika la Kimataifa la Oxfam imesema, viongozi wa utawala wa Kizauni wanaendelea kuzuia kuingizwa Gaza tani elfu 63 za bidhaa za chakula ambazo zilitazamiwa kutumwa kuwasaidia watu milioni 1.1. Kiasi hiki cha misaada ya chakula kilitosha kudkidhi mahitaji ya watu kwa angalau miezi miwili hadi mitatu lakini lori zlizobeba misaada hiyo zimezuiwa mpakani kutokana na mzingiro wa karibuni wa siku 23 uliowekwa na Israel.
342/
Your Comment