28 Machi 2025 - 17:38
Source: Parstoday
Mamilioni ya Wairani washiriki maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds

Wananchi Waislamu wa Iran kote nchini wamejitokeza kwa mamilioni kushiriki katika maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds, kuonyesha mshikamano na Palestina, na kulaani ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina hasa katika Ukanda wa Gaza.

Brigedia Jenerali Ramezan Sharif, Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) na Mkurugenzi Mkuu wa kamati ya Intifadha mjini Tehran, alitangaza hapo awali kwamba, mikusanyiko ya kuiunga mkono Palestina nchini Iran itaanza saa nne asubuhi kwa saa za hapa nchini, na yanafanyika katika miji zaidi ya 900 kote nchini.

Waliaondaa maandamano ya hapa Tehran tayari wameanisha barabara kadhaa kuu ambazo zinatumiwa na waandamanaji wa Kiirani wanaotaka kutuma ujumbe kwa jamii ya kimataifa juu ya hali ngumu ya maisha ya Wapalestina, na vile vile kuutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ukomeshe jinai na dhulma unazowafanyia wananchi hao madhulumu wa Palestina huko Gaza.

Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hayati Imam Ruhullah Khomeini (MA) kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds, kwa shabaha ya kuwatetea watu wanaodhulumiwa wa Palestina na kupigania ukombozi wa Quds Tukufu. 

Mamilioni ya Wairani washiriki maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds

Jana usiku, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisema maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu yanayofanyika leo Ijumaa ya Machi 28 kote duniani yatakuwa ya aina yake na yana umuhimu mkubwa kuliko miaka iliyopita.

Mikusanyiko hiyo ya hadhara ya Siku ya Quds inafanyika katika nchi nyingi za eneo la Asia Magharibi, zikiwemo Iraq, Yemen na Lebanon. Hali kadhalika, maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds yanafanyika katika pembe mbali mbalii za dunia, zikiwemo nchi za Afrika.

Mwandishi wa Radio Tehran akiwa jijini Dar es Salaam, Tanzania amesema umati mkubwa umejitokeza kwa hamasa kushiriki matembezi ya amani ya Siku ya Kimataifa ya Quds.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha