Leo Ijumaa Machi 28,2025 inasadifiana na Ramadhani 27 mwaka 1446 Hijria ni Siku ya Kmataifa ya Quds.
Imam Khomeini aliitangaza Ijumaa ya mwisho ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa Siku ya Kimataifa Quds ili Waislamu na wapenda haki kote duniani wajitokeze kwa wingi katika siku hiyo katika maandamano na mijumuiko ya kuunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina sambamba na kuulaani utawala wa Kizayuni wa Israel unaozikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
Ayatullah Nasser Makarim Shirazi katika ujumbe wake wa kulaani jinai za utawala bandia wa Kizayuni, ametaja maadhimisho makubwa ya maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kuwa ni chimbuko la faraja na nguvu kwa Mujahidin na madhulumu wa Palestina na Lebanon na kusisitiza kwamba, mtu yoyote hapasi kughafilishwa na jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni.
Naye Ayatullah Hussein Nouri Hamedani ameashiria kushtadi jinai za utawala wa haramu wa Kizayuni na kimya cha jamii ya kimataifa mkabala wa jinai hizo na kusema: Kwa mara nyingine tena mataifa ya Kiislamu duniani yatadhihirisha umoja na mshikamano wao dhidi ya jinai za utawala huo katili na waungaji wake mkono.
Wakati huo huo Ayatullah Jaafar Subhani pia amewatolea wito wananchi kuhudhuria matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Quds Duniani na akasema: Inafaa kwa wananchi wa Iran kushiriki katika maandamano ya Siku ya Quds Duniani kama ilivyokuwa miaka iliyopita na kukata mikono ya madhalimu mkabala wa Quds Tukufu.
342/
Your Comment