Yemen imefanya mamia ya operesheni dhidi ya maeneo na vituo mbalimbali vya Israel tangu kuanza kwa mashambulizi ya kijeshi ya utawala huo haramu dhidi ya watu wa Gaza zaidi ya mwaka mmoja uliopita, ambayo yameuwa zaidi ya Wapalestina 50,200 katika eneo hilo.
Abdul-Malik al Houthi amesema katika hotuba kwa wananchi sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds kwamba: "Haiwezekani kwa Yemen kutupilia mbali misimamo yake mbele ya hujuma na uvamizi wa Marekani, haijalishi chokochokozo hizo zitakuwa kubwa kiasi gani.
Amesema, mashambulizi ya Marekani dhidi ya Yemen hayawezi kuhalalishwa. Abdul -Malik al Houthi ameongeza kuwa: "Misimamo yetu dhidi ya adui Israel siku zote ipo wazi na vikosi vya ulinzi vya Yemen vinapambana dhidi ya mashambulizi ya Washington".
Kiongozi wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema, hakuna mantiki nyuma mashambulizi dhidi ya Yemen yanayotekelezwa na Marekani kwa sababu yanajiri kinyume na katiba ya Marekani.
Katika hotuba yake hiyo kwa wananchi wa Yemen, Abdul-Malik al Houthi amewatolea wito Wayemeni wote kushiriki kwa wingi katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Quds.
342/
Your Comment