28 Machi 2025 - 17:43
Source: Parstoday
Radiamali ya Hamas kufuatia kuuliwa shahidi "Abdel-Latif al-Qanoua" katika hujuma ya Israel

Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imeashiria katika taarifa yake kuhusu kuuawa shahidi Abdel-Latif al-Qanoua Msemaji wa harakati hiyo katika shambulio la utawala wa Kizayuni na kutangaza kuwa: "Kuwalenga kwa masambulizi viongozi wa harakati ya Hamas na wasemaji wake kamwe hakuwezi kuvunja irada yetu.

Katika taarifa yake, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imepongeza jitihada za mapambano ya shahidi Abdel-Latif al-Qanoua Msemaji wa harakati hiyo katika kuwahami na kuwatetea wananchi na malengo ya Palestina na kusisitiza kuwa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya viongozi wa muqawama abadan hayatavunja azma na irada ya Wapalestina; na kwama damu ya mashahidi hao itaendelea kuwa ilhamu ya mapambano hadi kupatikana ushindi. 

Harakati ya Hamas jana Alhamisi ilitoa taarifa na kuthibitisha kuuawa shahidi msemaji wake Abdel-Latif al-Qanoua katika shambulio la moja kwa moja la jana asubuhi lililotekelezwa na utawala wa Kizayuni dhidi ya mahema yanayowahifadhi wakimbizi wa Kipalestina katika mji wa Jabalia huko kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. 

Hamas imesema, shahidi al Qanoua alikuwa imara na ngangari tangu adui Mzayuni aanzishe mashambulizi ya kikatili na mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza. 

Taarifa ya Hamas imesisitiza kuwa: Shahidi al Qanoua alikuwa kigezo cha kigezo cha siku zote na alijitolea maisha yake katika kuwatumikia watu na kadhia ya Palestina.

Tovuti ya televisheni ya al Mayadeen imeripoti kuwa, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imesisitiza katika taarifa yake kuwa: Mashambulio ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya viongozi wa Hamas na wasemaji wake kamwe hayatavunja azma na irada ya harakati hiyo ya mapambano; bali yatazidisha mashinikizo ya yao kwa ajili ya kuendelea njia hiyo hadi kukombolewa ardhi na matukufu ya Palestina. " Damu ya mashahidi hawa wa Palestina itatoa msukumo na kuwa ilhamu ya mapambano hadi kupatikana ushindi dhidi ya Wazayuni maghasibu," imeongeza taarifa ya Hamas. 

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha