28 Machi 2025 - 17:44
Source: Parstoday
Yemen yautwanga kwa makombora utawala wa Kizayuni/sauti za ving'ora zasikika

Duru za Kizayuni zimearifu kuwa sauti za ving'ora vya hatari vilisikika jana katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) kufuatia shambulio la makombora ililotekelewa na jeshi la Yemen.

Duru hizo pia ziliripoti kwamba ving'ora vilisikika huko Tel Aviv na Quds na kkatikati ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavuhuku milio ya milipuko ikisikika huko Quds. Pia, vyanzo hivyo vya Kizayuni pia vilidai kuwa utawala wa Israel ulifanikiwa kusambaratisha makombora 2 yaliyorushwa kutoka Yemen.

Kanali ya 14 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni ilitangaza kuwa kombora moja lilivurumishwa kuelekea maeneo ya katikati mwa Israel kutoka Yemen. 

Msemaji wa jeshi la utawala ghasibu wa Kizayuni pia ametangaza kuwa ving'ora vya hatari vilisikka katika baadhi ya maeneo ya Israel kutokana na kuvurumishwa makombora kutoka Yemen. 

Hii ni katika hali ambayo kanali ya 13 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni pia ilitangaza kufuatiliwa kwa karibu makombora mawili yaliyorushwa na jeshi la Yemen kuelekea maeneo ya katikati ya utawala wa Kizayuni. Televisheni ya al Arabi pia ilitangaza kuwa sauti za milipuko zilisika katika maeneo ya Bait Laham na kaskazini mwa al Khalil. 

Wakati huo huo kanali ya 13 ya televisheni ya utawala wa Kizayuni imetangaza kuwa mabaki ya makombora yameangukia karibu na kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha "Mifu Huron" karibu na mji wa Ramallah.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha