6 Juni 2015 - 18:49
 Serikali ya Marekani inapinga Rais Kagame kugombea tena Urais wa Rwanda

Mwanadiplomasia wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Marekai ameliambia shirika la habari la AFP kwamba

Mwanadiplomasia wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Marekai ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, nchi hiyo itapinga hatua zozote za kumruhusu rais wa Rwanda Paul Kagame kuwania urais kwa muhula mwengine wa tatu. Mwanadiplomasia huyo amesema Marekani ina nia ya kuunga mkono makabidhiano ya madaraka kwa njia ya demokrasia kwa rais mpya atakayekuwa amechaguliwa na Wanyarwanda. Katiba ya Rwanda ya mwaka 2003 inamruhusu rais kugombea kwa vipindi viwili tu hatua inayomnyima Rais Kagame aliyechaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 2003, na kisha mwaka 2010, nafasi nyengine ya kugombea urais. Hata hivyo wiki iliyopita maafisa wa Rwanda walisema katika miezi miwili ijayo bunge la nchi hiyo litajadili mabadiliko ya katiba ili Kagame aweze kugombea tena urais, jambo ambalo washirika wa rais huyo wa Rwanda wanasema limetokana na matakwa ya wengi.