Jeshi la anga la Israel limesema limeushambulia Ukanda wa Gaza mapema leo hii kwa mara ya pili ndani ya siku tatu kufuatia kufuatia kile wanachokiita kuvurumishwa upya kwa roketi kaskazini mwa Israel kutokea Gaza. Jeshi hilo limesema kombora hilo lilipiga eneo la wazi katika mji wa bandari wa Ashkelon eneo lililolengwa katika mashambulizi matatu ya roketi siku ya jumatano usiku. Hata hivyo hakuna majeruhi wowote walioripotiwa. Hali hiyo imesababisha Israel kujibu shambulizi kwa kuanzisha mashambulio ya anga ndani ya Ukanda wa Gaza. Serikali ya nchi hiyo pia imeamuru kufungwa mipaka yake ya Erez na Kerem Salom hadi hapo kutakapotolewa tangazo jengine.