27 Julai 2015 - 20:56
Rais wa Syria ahidi kuwashinda magaidi

Serikali ya Iran pamoja na kuwa na vikwazo vikali imekuwa mstari wa mbele katika kuzisaidia serikali za Syria na Iraq sizianguke katika mikono ya magaidi wanaungwa mkono na mataifa ya magharibi na washirika wao kwa lengo la kukuza utawala wao na kunyonya utajili wa mafuta kwa urahisi.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Katika hotuba yake ya kwanza hadharani katika kipindi cha mwaka mmoja Rais Bashar Assad wa Syria Jumapili ya jana tarehe 26 mwezi wa 7 mwaka 2015 ameapa kushinda vita vya vinavyosababishwa na makundi ya kigaidi yanayodhaminiwa na nchi za Maghalibi zikishirikia na baadi ya nchi za kiarabu kwa lengo la kuuangusha utawala wa rais huyo aliyepinga kuwa chini ya Marekani na washirika wake na badala yake kujiweka karibu na Jamhuri ya kiislamu ya Iran.  

Hotuba yake hiyo ilionyesha kujiamini imekuja mwaka wa tano wa mzozo unaowapambanisha vikosi vyake na vile vya maagaidi wa Kiislamu wa itikadi kali na Kundi la magaidi la itikadi kali la Daesh.

Hotuba hiyo ya Assad iliyoonyeshwa kwenye televisheni wakati wa asubuhi ni ya kwanza kutolewa hadharani tokea aapishwe kwa muhula wa tatu wa miaka saba madarakani hapo mwezi wa Julai mwaka jana.

Katika kipindi hicho Assad alifanya mahojiano na vyombo vya habari kadhaa vya Kiarabu na vya kimataifa.Assad amekiri kwamba magenerali wake ilibidi wahamishe vikosi vyake kutoka eneo moja la mapambano kwenda jengine ili kuyahami maeneo ambayo yana umuhimu kijeshi, kisiasa au kiuchumi.Amesema kwamba kutekwa kwa baadhi ya maeneo na magaidi hao wanaoungwa mkono na Marekani, na washirika wake kumewavunja moyo Wasyria.

Vikosi vya Syria vimepata pigo mara kadhaa tokea mwezi wa Machi ikiwa ni pamoja na kupoteza mji wa Idlib kaskazini magharibi ambao ni mji mkuu wa jimbo lenye kupakana na Uturuki ambayo imekuwa ikiwa saidia magaidi hao silaha na mafunzo ya kijeshi.

 Hapo mwezi wa Mei serikali ilipoteza mji wa kihistoria ulioko kati mwa nchi hiyo wa Palmyra kwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Daesh ambao pia waliteka sehemu ya mji wa kaskazini mashariki wa Hassakeh na majeshi Marekani yanayodai kupambana na  Magaifi hao yakitazama jinai hizo bila kuchukua hatua yeyote.

Kupoteza kwa miji hiyo kwa kiasi fulani kunaweza kusahihishwa hivi sasa kutokana na msaada mkubwa kutoka kwa mshirika mkubwa wa serikali Iran ambayo imefikia makubaliano ya nyuklia na nchi zenye nguvu duniani ambapo kwayo nchi hiyo itaondolewa vikwazo vya kimataifa iilivyowekewa.

Hotuba yake yashangiliwa

Assad ambaye alikuwa akikatizwa mara kwa mara kwa kushangiliwa katika hotuba yake hiyo amesema "Hatusambaratiki.Tuko imara na tutapata ushindi."

Amesema suala la kushindwa haliko katika kamusi ya jeshi la Waarabu wa Syria.

Assad amejaribu kuhalalisha kupoteza baadhi ya maeneo ukiwemo mji wa Idlib. Vikosi washirika wa Assad wakiwemo wapiganaji wa kundi la Hizbollah la Lebanon na wataalamu wa vita na masuala ya kijeshi wa Iran wanadhibiti eneo kubwa la nchi hiyo na kuvirudisha nyuma vikundi vya kigaidi zaidi ya 12 ambavyo vimepandikizwa na nchi za maghaaribi ili kuanguasha utawala wa Syria.

Amesema ilikuwa ni muhimu kuweka utulivu katika maeneo muhimu ili wanajeshi wao waendelee kuyashikilia na kwamba wasi wasi juu ya wanajeshi wao umewalazimisha wayaachie maeneo mengine.

Assad amekiri kwamba kuna uhaba wa askari jeshini lakini amesema hataki kutoa taswira mbaya ambayo itatumiwa na vyombo vya habari hasimu kusema kwamba rais anasema watu wanakwepa kujiunga na jeshi. Amesema katika miezi ya hivi karibuni hasa ya April ma Mei idadi ya watu wanaojiunga na jeshi imeongezeka na kwamba kila punje ya ardhi ya Syria ina thamani na itaokolewa.

Msamaha waliolikacha jeshi

Hapo Jumamosi serikali ya Assad imetangaza msamaha wa jumla kwa askari waliokimbia jeshini na watu wanaokwepa kujiandikisha jeshini kutimiza wajibu wao wa kutumikia taifa Kuna maelfu ya askari walioliasi jeshi ndani na nje ya Syria wengi wao wamejiunga kupambana upande wa magaidi wanaoungwa mkono na Marekani. Vijana wengine wengi wameikimbia nchi hiyo kuepuka kuadikishwa jeshini ambalo ni jambo la lazima.

Assad pia ametoa msamaha kama huo kwa wahalifu lakini hakuna mfungwa yoyote wa kisiasa aliyeachiliwa huru miongoni mwa maelfu ya wafungwa wa kisiasa walioko magerezani nchini Syria.

Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu nchini Syria lenye makao yake nchini Uingereza hivi karibuni limeripoti kwamba takriban wanajeshi 49,100 na wapigananji 32,500 wanaoiunga mkono serikali wameuwawa tokea uasi ulipoanza nchini humo hapo mwezi wa Machi mwaka 2011.

Assad amesema serikali yake ilikuwa haikuvitaka vita hivyo lakini kutokana na kwamba vililazimishwa kwao jeshi la Waarabu wa Syria lilikabiliana na magaidi wanaotumwa na nchi za Magharibi popote watakapokuwa.

Akizungumzia juu ya mazungumzo ya kisiasa kiongozi huyo wa Syria amesema juhudi zozote zile ambazo hazizingatii kupambana na ugaidi zitakuwa hazina maana yoyote ile.

Serikali ya Iran pamoja na kuwa na vikwazo vikali imekuwa mstari wa mbele katika kuzisaidia serikali za Syria na Iraq sizianguke katika mikono ya magaidi wanaungwa mkono na mataifa ya magharibi na washirika wao kwa lengo la kukuza utawala wao na kunyonya utajili wa mafuta kwa urahisi.