12 Agosti 2015 - 20:18
 NATO yakana kuchochea vita barani Ulaya

Shirika la kujihami la NATO leo limetetea mazoezi yake kadhaa inayofanya kujibu uvamizi wa Urusi unaoongezeka na kupanusha wazo kwamba shirika hilo linasaidia kutayarisha vita katika bara la Ulaya.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Shirika  la  kujihami la  NATO  leo  limetetea  mazoezi  yake kadhaa  inayofanya  kujibu  uvamizi   wa  Urusi unaoongezeka  na  kupanusha  wazo  kwamba  shirika  hilo linasaidia  kutayarisha  vita  katika  bara la Ulaya.

Umoja  huo  ulikuwa  ukijibu  onyo  kutoka  chombo cha kutoa  mawazo  mjini  London  juu  ya  hatari  ya  ongezeko kubwa  nchini  Urusi  na  NATO  la  mazowezi  ya  kijeshi tangu mzozo  kati  ya  serikali  ya  Ukraine  na  wapiganaji wanaotaka  kujitenga  wanaounga  mkono  Urusi  kuzuka mwezi  Aprili  mwaka  jana.

Msemaji  wa  NATO Carmen Romero  amesema  baada  ya kuchapishwa   tathmini  hiyo  na  mtandao  wa  uongozi barani  Ulaya  ELN, kwamba  mazowezi  ya  kijeshi  ya NATO sio  kama  inavyoripotiwa  kwamba  yanakaribisha uwezekano  wa  vita  barani  Ulaya.

Badala  yake  amesema  yanafanya  kinyume   na  hivyo, kuimarisha  usalama  na  uthabiti  katika  bara  la  Ulaya kutokana  na  uvamizi  unaoongezeka  wa  Urusi.

Mwisho wa habari/ 291