Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Ujerumani imesisitiza kuwa hatua ya Shirika la Fedha Duniani-IMF kuunga mkono mpango wa tatu wa uokozi wa Ugiriki ni muhimu kwa nchi hiyo kuunga mkono makubaliano. Christiane Wirtz, msemaji wa Kansela Angela Merkel, amesema ushiriki wa IMF ni muhimu kwa serikali hiyo na suala hilo halijabadilika. IMF, mmoja wa wakopeshaji wa Ugiriki, ilisema inawataka washirika wa Ulaya wa Ugiriki kukubaliana kuhusu msaada wa fedha za uokozi kabla hawajaamua kama itashiriki katika mpango mpya wa uokozi. Wakati huo huo Waziri wa Fedha wa Ujerumani, Wolfgang Schaeuble ameelezea matumaini yake kwamba yeye na mawaziri wenzake wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro, watauidhinisha mkopo wa tatu wa uokozi kwa Ugiriki, katika mkutano wao wa leo mjini Brussels.
Mwisho wa habari/ 291