Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: mripuko huo mkubwa uliotokea mjini Ankara umesababisha hasara kubwa sana nchini humo, tukio hilo limetokea katika moja ya vituo vya treni viliopo katikati mwa mji huo nchini Uturuki.
Aidha tukio hilo limetokea katika hali ambayo mashirika kadha yasiokuwa ya kiserikali (umoja wa Madaktari, umoja wa wahandisi, umoja wa wafanyakazi) kutaka kufanya maandamano ambayo yalikuwa na anuani ya (mjumuiko wa amani) ambayo ni dhidi ya siasa za kivita za viongozi wa Uturuki (Rajab Tayyip Erdogan na Ahmad Daud Ughlu).
Vyombo vya habari vya uturuki vikunukuu kutoka katika wizara ya mambo ya ndani vimetangaza idadi ya walio uwawa katika tukio hilo kufikia watu 86 na wengine 186 kujeruhiwa, huku baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo waeleza kuwa mripuko huo ulitokea mara mbili sehemu hiyo.
Viongozi wa serikali ya Uturuki wametangaza kuwa: mripuko wa Ankara unatokana na vitendo vya kigaidi na kuhusu tukio hilo uchungunzi bado unaendelea kufanywa.
Kamal Kilicdaroglu (kiongozi wa chama Republican nchini humo) ametoa ujumbe mkali kuhusu tukio hilo huku akisema: vitendo vya ugaidi vimesambaa katika ukanda wa mashariki ya kati na sasa umewasili nchini Uturuki.