Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Utawala wa kifalme ya Saudia Arabia imetangaza kumnyonga mwanaharakati wan chi hiyo aliyekuwa akitetea haki za wananchi wa nchi hiyo.
Serikali ya Utawala wa kifalme ya Saudia Arabia imetangaza kumnyonga Sheikh Nimr ambaye ni mwanaharakati aliyekuwa akitetea haki za waislamu wa dhehebu la Shia wanaoishi katika nchi hiyo.
Utawala wa Saudia arabia umekuwa ukitumia fedha nyingi kuleta sintofahamu na tofauti kati ya dhehebu la Sunni na Shia duniani.
Saudia abia imbayo inaongozwa na waislamu wa dhehebu la Wahabia imekuwa ikifanya ukatili na dhulma kwa waislamu wa dhehebu la Shia wa Saudia arabia na hata wa nje ya nchi hiyo.
Saudia arabia ndio mdhamini mkuu wa makundi ya kigaidi yanayopigana nchini Iraq na Syria ikiwemo kundi la kigaidi la Daesh na mengineyo.
Serikali ya Saudia arabia imetangaza kumnyonga mwanaharakati huyo, pamoja na watu wengine 46.
Mwanaharakati huyu amehukumiwa hukumu ya kifo billa hata ya kupewa haki ya kujitetea au haki ya kuwa na wakili.
Kuuawa kwa mwanaharakati huyu kumepelekea maandamano makubwa mashariki mwa Saudia arabia sehem ambako kunaishi waislamu wengi wa dhehebu la Shia.
Kuawa kwa mwanaharakati huyu huenda kukaleta hatari kubwa na hasara isiyokuwa na fidia kwa utawala wa kifalme wa Saudia arabia.
Mwisho wa habari/ 291