11 Januari 2016 - 20:44
Msafara wa misaada ya kibinadamu wawasili Syria

Msafara wa msaada wa chakula na madawa Jumatatu ya leo tarehe 7 mwezi wa 1 mwaka 2016 umewasili katika vituo vya ukaguzi vya serikali nje ya mji wa Madaya uliozingirwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na wafuasi wake nchini Syria ambapo takriban watu 30 wamekufa njaa.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Msafara wa msaada wa chakula na madawa Jumatatu ya leo tarehe 7 mwezi wa 1 mwaka 2016 umewasili katika vituo vya ukaguzi vya serikali nje ya mji wa Madaya uliozingirwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na wafuasi wake nchini Syria ambapo takriban watu 30 wamekufa njaa.

Msafara wa Umoja wa Mataifa wa chakula na madawa umewasili nje ya mji huo uliozingirwa ukiwa na magari 40 yanayosubiri kuingia.

Msafara huo hautovuka kuingia Madaya hadi hapo msafara sanjari na huo utakapoweza kuingia katika miji miwili ya wakaazi wa Kishia inayoshikiliwa na serikali na kuzingirwa na Magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na Saudia arabia kaskazini magharibi ya Syria.

Duru kutoka chama cha hilali Nyekundu cha Syria imesema takriban tani 330 za msaada wa chakula na madawa zinapelekwa katika mji wa Madaya na unaweza kutumika kwa siku 40.

Mji huo ulioko kama kilomita 25 kaskazini mwa mji mkuu wa Damascus ambao umetekwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani umekuwa ukizingirwa tokea mwezi wa Julai na vikosi vilivyo tiifu kwa Rais Bashar al Assad vikisaidiwa na wanamgambo wa kundi la Hezbollah katika juhudi za kuhakikisha kwamba magaidi hao wanaoungwa mkono na Marekani wasiweze kutoka bila ya kutiwa nguvuni, ndege za Marekani zimekua zikijaribu kuwapelekea misaada na silaha magaidi hao lakini kwa sasa imeshindikana kutokana na uwepo wa majeshi mahili ya Syria.

Wakaazi wanakufa njaa na kukabiliwa na ukatili wa magaidi

Zaidi ya watu 20,000 hivi sasa wamekwama ndani ya mji huo wa Madaya kwa mijibu wa Shirika la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka ambalo limesema watu wengine watano wamekufa njaa wakati wa usiku.

Wiki iliopita shirika hilo limesema watu 23 wamekufa njaa katika hospitali ya mji huo ambayo imekuwa ikiisaidia tokea mwanzoni mwa mwezi wa Disemba.

Vijiji vya waislamu wa dhehebu la Shia vya Foua na Kafraya vilioko kaskazini magharibi mwa jimbo la Idlib vimekuwa vikizimgirwa na waasi tokea mwezi wa April.Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu nchini Syria limesema mtu mmoja amekufa kutokana na uhaba wa chakula na madawa katika vijiji hivyo.

Saudia arabia ambayo ndio msaidizi mkuu wa makundi ya kigaidi imekuwa ikijaribu kutuma makundi ya kigaidi ili kukabiliana na majeshi ya Syria yanayolinda mji huo ili magaidi hao wapate kutoka lakini imeshindikana pia, umoja wa mataifa umeongea na magaidi hao na kuwa hamisha baadhi ya magaidi hao ili wakapate matibabu nchini Uturuki ambapo magaidi wengi wanapata mafunzo ya kijeshi.

Kukomesha mauaji ya raia

Ikiwa zimebaki kama wiki mbili kabla ya kuanza kwa mazungumzo ya kutafuta usuluhishi kwa mzozo huo wa Syria waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius ameendeleza madai yake yasiyo na mashiko yakuzitaka Urusi na Syria kukomesha operesheni zao za kijeshi dhidi ya raia na hususan kukomesha maafa yalioko katika mji wa Madaya na miji mengine iliozingirwa nchini humo kutokana na vituo vya ukaguzi vya serikali.

Fabius amesema "Tumezungumzia umuhimu mkubwa kwa Syria na Urusi kuzuwia opesheni zao za kieshi dhdi ya raia. Nimetaja miji miwili tu lakini kuna miji mengine na hususan maafa katika mji wa Madaya na miji mengine ya Syria inayozingirwa na vikosi vya serikali kutokana ukaguzi wa vituo vyake."

Ufaransa ambayo mpaka sasa haijulikani iko upande gani kwani imekuwa ikipinga utawala halali wa Bashar asad na katika siku za karibuni imejikuta ikijinadi kutaka kupambana na magaidi kufuatia mashambulizi ya kigaidi nchini Ufaransa.

Shirika la Madaktari wasiokuwa na Mipaka limeonya kwamba usambaazaji wa chakula na madawa katika mji wa Madaya unatakiwa kufanyika kwa kawaida na kwamba mkupuo mmoja wa misaada hiyo hautoshi.

Mwisho wa habari/ 291