Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: msikiti mmoja umeripuliwa na mabomu katika maeneo wanaishi wafuasi wa madhehebu ya kishia mashariki mwa Saudi Arabia.
Shambulio hilo la kigaidi limefanyika siku ya Ijumaa katika msikiti mmoja uliopo katika wilaya Mahasin mkoani Al-Hasa, huku habari za awali zinaeleza kuwa watu watatu wamepoteza maisha kutokana na shambulio hilo.
Kwa mujibu wa habari ziliotangazwa katika tukio hilo zinasema kuwa awali kulitokea mripuko ndani ya msikiti huo kisha watu 5 waliokuwa na silaha wakaanza kushambulia katika msikiti huo, huku wakirushiana risasi na majeshi ya ulinzi waliokuwa sehemu hiyo.
Televisheni ya Aljazira imetangaza kuwa polisi wa Saudi Arabia wamefanikiwa kuwakamata watu wawili baada ya mashambulio hao.
mwisho wa Habari/290