Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Kiongozi wa kundi kuu la upinzani la Syria Riad Hijab ametua leo nchini Uswisi kujaribu kuvunja mkwamo wa mazumgumzo ya amani
Hayo ni wakati serikali ya Urusi ikiapa kuwa haitasitisha mashambulizi yake ya angani dhidi ya magaidi wanaoungwa mkono na Saudia arabia na Marekani ambao wameitaka Urusi iache kushambulia magaidi ili mazungumzo yaendee.
Urusi imesititiza kwamba itaendeleza mashambulizi dhidi ya magaidi na itaendelea kuunga mkono utawala halali wa Rais Bashar al-Assad.
Juhudi za kubwa kabisa kufikia sasa za kujaribu kumaliza vita vilivyodumu miaka mitato kutokana na uchochezi wa mataifa ya nje yakiongozwa na Marekani na Saudia arabia nchini Syria. Juhudi hizo zilitumbukia katika mkanganyiko hapo jana baada ya upinzani kuufuta mkutano wake na mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Staffan de Mistura katika hatua ya kukasirishwa na mamia ya mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Urusi dhidi ya magaidi tangu Jumatatu.
Wawakilishi wa serikali ya Rais Bashar al-Assad waliikemea Kamati Kuu ya Majadiliano – HNC ambalo ndilo kundi kuu la upinzani, wakisema halina mwelekeo na lililojaa magaidi, wakati likitofautiana na de Mistura kuwa mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja tayari yameanza.
Upande wa upinzani unamtaka Assad kuruhusu uingizaji wa misaada ya kiutu katika miji iliyozingirwa, kukomesha mashambulizi ya mabomu dhidi ya magaidi na kuwaachia maelfu ya wafungwa wa kigaidi wanaoendelea kuteseka katika magereza ya serikali.
Serikali ya Syria inasema upinzani umeshindwa kuwasilisha hata orodha ya wajumbe wake na inapinga vikali kujumuishwa kwa waasi ambao wanaonekana kuwa ni magaidi.
Mmoja wa viongozi kama hao ni Mohammed Alloush, mwanachama mkuu wa kundi la magaidi wa la Jeshi la Kiislamu, ambaye amekuwa Geneva tangu Jumatatu na kawaida huwa mjumbe mkuu wa upinzani ambaye amesema leo kuwa “hana matumaini” kuhusu mazungumzo hayo.
Naye mkuu wa ujumbe wa serikali katika mazungumzo hayo Bashar al-Ja'afari amesema awamu ya maandalizi ya mazungumzo hayo ya Geneva huenda ikachukua muda mrefu zaidi kuliko ilivyotarajiwa.
De mistura amesema ikiwa mazungumzo haya yatakwama, “matumaini yote yatakuwa yamepotea”. Kiwango cha uaminifu kinakaribia sifuri baina ya pande zote mbili. Kiwango cha uhasama baina ya pande zote ni kikubwa mno. Na hisia ya uharaka ambayo sote tunaihisi, pia ipo nao kwa sababu wanafahamu kuwa mzozo huu umedumu muda mrefu. Hivyo tulipo kwa sasa ni katika hatua ya maandalizi kwa ajili ya mazungumzo halisi.
Aidha amesema kuwa “kiwango cha matumaini baina ya pande mbili zinazoshiriki katika mazungumzo kinakaribia sifuri”.
Mashambulizi ya karibuni ya Urusi dhidi ya magaidi tangu nchi hiyo ilipotangaza kumuunga mkono kijeshi rais Assad mwishoni mwa mwezi Septemba yaliwaruhusu wanajeshi watiifu kukaribia kuvunja vizuizi vilivyowekwa na magaidi katika vijiji viwili vinavyodhibitiwa na serikali karibu na mji wa Aleppo.
Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Urusi Sergei Lavrov amesema leo kuwa haoni haja yoyote ya kusitishwa mashambulizi ya angani, huku akiwashutumu magaidi katika upande wa upinzani na kile alisema ni uingizaji silaha Syria kutokea Uturuki.
Habari iliyotufikia hivi sasa ni kwamba majeshi ya Syria yamefanikiwa kuvunja vizuizi vya magidi na kuogoa maelefu ya wananchi waliokuwa wamezingirwa na magaidi hao, kwa sasa magaidi wanajikuta hawana hoja katika vikao vya kutafuta amani.
Mwisho wa habari/ 291