17 Februari 2016 - 16:40
Umoja wa mataifa wataka mazungumzo ya  amani ya Syria

Uturuki ambayo ndio lango kuu la kuingiza magaidi na silaha nchini Syria na Iraq imejikuta kwenye kipindi kigumu baada ya ishara kuonyesha kuwa jeshi la Syria litashinda vita dhidi ya magaidi hao, hivyo inapata wasiwasi kwani imetumia juhudi zote ikishirikiana na Marekani na wafuasi wao kuhakikisha kuwa serikali halali ya Syria inaaguka.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema mjumbe maalum wa Umoja huo kwaajili ya Syria Staffan de Mistura amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Syria, yanayonuiwa kusitisha mapigano yaliyodumu kwa miaka mitano yanayosababishwa na magaidi wanaoungwa mkono na Marekani na washirika wake.

Msemaji huyo wa Umoja wa Mataifa Ahmad Fawzi amesema, Staffan de Mistura anatarajiwa kukutana kwa mara ya pili na Walid al-Moualem baadaye leo mjini Damascus kujadili kuanzishwa tena mazungumzo ya amani yanayotarajiwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu wa Februari, baada ya duru ya kwanza ya mazungumzo kuahirishwa wiki iliyopita.

Katika taarifa fupi aliyoitowa kwa waandishi habari baada ya mkutano wao wa kwanza, de Mistura aliweka wazi yale waliyoyazungumza pamoja na Waziri Moualem.

"Tumekuwa tukizungumzia masuala ya upatikanaji wa misaada ya kibinaadamu kwa maeneo yote yaliyozingirwa sio tu na serikali lakini pia na upinzani na magaidi wa Daesh," alisema de Mistura.

Serikali ya Uturuki yaishutumu Urusi kutekeleza uhalifu wa kivita

Wakati huo huo Uturuki hapo jana iliishutumu Urusi kutekeleza uhalifu wa kivita, baada ya mashambulizi ya maroketi Kaskazini mwa Syria, kusababisha vifo vya takriban watu 50, huku ikitoa onyo kwa wapiganaji wa kikurdi kwamba watapambana na majibu makali kutoka iwapo watajaribu kuudhibiti mji uliyoko karibu na mpaka wake.

Uturuki ambayo ndio lango kuu  la kuingiza magaidi na silaha nchini Syria na Iraq imejikuta kwenye kipindi kigumu baada ya ishara kuonyesha kuwa jeshi la Syria litashinda vita dhidi ya magaidi hao, hivyo inapata wasiwasi kwani imetumia juhudi zote ikishirikiana na Marekani na wafuasi wao kuhakikisha kuwa serikali halali ya Syria inaaguka.

Mwisho wa habari/ 291