Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Serikali ya Ujerumani imeitaka Ufaransa kufunga kinu chake cha nyuklia cha Fessenheim kilicho karibu na mpaka wake haraka iwezekanavyo.
Tamko hili linafuatia ripoti za vyombo vya habari nchini Ujerumani, kwamba tukio la kuvuja kwa maji kutoka moja ya mitambo ya kinu hicho mwezi Aprili 2014, lilikuwa kubwa zaidi kuliko lilivyoripotiwa.
Msemaji wa wizara ya mazingira nchini Ujerumani, alisema tukio hilo lilijadiliwa kwenye kikao kati ya nchi hizo mbili wakati huo.
Stefan Haufe anasema Ujerumani inakubaliana na tathmini ya Ufaransa juu ya ukubwa wa tukio hilo, lakini ina mashaka na ukongwe wa kinu hicho, kilichoanza kazi mwaka 1977.
Haufe amesema hivi leo kwamba matukio ya aina hiyo si mara ya kwanza kutokea na ndio maana Ujerumani inataka kifungwe haraka iwezekanavyo.
Mwisho wa habari/ 291