Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Jeshi la Syria limegundua kaburi la pamoja likiwa na miili yawatu 42 na wanajeshi waliouwawa na Kundi la kigaidi la Daesh mjini Palmyra. Chanzo cha kijeshi kimetoa taarufa kwamba kaburi hilo lilikuwa na miili ya wanajeshi, wanachama wa kamati maarufu za usalama mjini humo na jamaa zao na kuongeza kwamba maiti 24 zilikuwa za raia. Miili ya watu hao imepelekwa katika hospitali ya mji mkuu wa jimbo wa Homs na mingine kutambuliwa. Jumapili iliyopita Jeshi la Syria lililokuwa likiungwa mkono na jeshi la Urusi na kusaidiwa na wataalamu wa vita kutoka Iran lilifanikiwa kuukomboa mji wa Palmyra uliyo katika urodha ya turathi ya UNESCO ambao ulitekwa na Kundi la kigaidi la Daesh Mei 2015, wakati ambapo majeshi ya Muungano wa Marekani yakiwa yanatazama kundi hilo likichukua mji huo na kuua watu kiholela, huku majeshi hayo yakirusha ndege zake katika anga hilo, jambo ambalo limefasiriwa na wengi kuwa ilikuwa ni njama ya kuyasaidia makundi hayo ya kigaidi kusonga mbele bila ya kushambuliwa na ndege za majeshi yaserikali ya Syria. Kwa mujibu wa Shirika la Uangalizi wa Haki za Binaadamu la Syria lenye makao yake makuu nchini Uingereza, kundi la kigaidi la Daesh limeuwa watu 280 katika harakati za kuudhibiti mji huo.
Mwisho wa habari/ 291